Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, September 15, 2018

Kuwa mpenzi wa mtu sio tu zawadi ni KIPAJI | love ma woman


Unatambua kuwa nimekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya miongi miwili sasa. ?
Kuwa mpenzi wa mtu sio tu zawadi ni KIPAJI na zaidi ya mafunzo
(Copy that 👆👆)
Katika kipindi chote hicho cha mahusiano kuna mambo kadhaa nimejifunza.
Nimejifunza kuwa
Jukumu kubwa la mimi kama mpenzi wa mtu ni KUPENDA,KUJALI NA kumlinda mwenza wangu katika kipindi chote cha uwepo wake.Na zaidi kumjengea hisia za kuwa na uweZo na kujiamini.
Niamini (ila sio lazima) kama utamjengea mwenza wako mazingira ya kuwa na hofu na wewe hakuna furaha ya mahusiano. Wala upendo wa dhati.
NIMEJIAMINI,NIMEJIPENDA
Hujipendi wala kujiamin ni ngumu kutoa Upendo na uaminifu kwa mwingine.
Hivyo ndivyo ninavyoamini mimi
Yaani natimiza wajibu kabla ya kudai haki.
NIMEISHINDA TAMAA
Wengi wanaimani potofu kuwa wanawake wapo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya mwili na fikra zake tu.
Ila mimi Sijawahi kufikiria hivyo kwanza
Kuna vitu vingi nahitaji kutoka kwake. Mawazo yake ni muhimu sana kwangu na familia yetu.
Kumbuka
MPENZI WAKO SIO MALI YAKO.
Mwanzo mzuri ulionipa matokeo ya mahusiano imara na yenye furaha nilitambua mapema kuwa mpenzi wangu sio mali yangu. Ni mali yake yeye mwenyewe.Yeye ni zawadi toka kwa mungu.
MPENZI WAKO NI ZAWADI YA THAMANI SANA.
Pindi nilipoanza kumuona mwenza wangu kama zawadi ya thamani
Nilianza kuona majukumu yangu ya kimahusiano kwenye mtazamo tofauti kabisa.
Na sasa
Nafurahia na kushawishi mazingira ya utu kwake nataka mahusiano yangu yachanue kama maua.
Sitaki niwe chanzo cha mwenza wangu kukosa furaha . Sihitaji mahusiano yangu kuanguaka.
Dhana moja ya kuboresha mahusiano yangu yametegemea kiasi cha upendo anachopokea mwenza wangu kutoka kwangu.Ama upendo niliowekeza kwake.
Wapendwa
Wenza wetu wanahitaji upendo wa vitendo si tu wa maneno. kama vile maua yanavyohitaji maji. Zaidi ya hapo utamtengenezea mtu mateso na majuto tu.
Na tegemea mahusiano yako kuanguka kama jani la mti majira ya kiangazi.
_______________

No comments:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages