najua michakato ya maisha ndio inatufanya tuwaachie mabibi rundo la vijikuu kule ma home
haikatazwi wala haigombwi
vp lakini yule mtoto kule kijijini anakula, kulala na kuvaa vizuri kama wewe huku mjini?
hapendezi
mama akulee wewe kwa shida na amlee mwanao pia kwa shida
usijisifu tu kwamba hata wewe ni mama au baba fulani
wakati huyo fulani mwenyewe anatembea pekua TAKO nje plus utapiamlo.
tusake mkwanja ila na ufalme wa mbingu pia tusiusahau.
mungu anakuona jinsi unavyomfanya malaika wake.
tuisadie serikali kupunguza na kuondoa kabisa watoto wa mitaani,kila mzazi ashiriki kikamilifu jukumu la malezi ya mwanae.
No comments:
Post a Comment